THE SWAHILI LOVE LETTER

​6/11/2016
Mpenzi wangu Le Sucre, 
Habari za kushinda mboni ya jicho langu, 

Kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu,

Nattamai u buheri wa afya,

Nimekuhata mithili ya nyuki kuhata maua,

Nimehata tabasamu lako ambalo ndio nalipenda zaidi, 

Kila mara huwa nalihisi liko mbeleni mwangu,

Kicheko chako ambacho nikisikia moyo wangu unashikwa na furaha,

Huzuni unishika kwa kuwa muda mwingi uko mbali,

Kabla nisahau wape salamu zangu baa mweke na mashemeji,
Leo nimeona nikuandikie arafa kwa kiswahili,

Manake nimekaa huku  uswahilini kwa mda,

Nimeona ni bora nitumie lugha ya wahenga,

Kiswahili kigumu lakini bidii ya mchwa ntatia,

Nachukua hatua, ila wenyeji bado wananikejeli,

Si heri kusema ninakengeuka, bali ninajifunza mambo fasaha mawili, matatu,
La kwanza la husu Ustaarabu, 

Ustaarabu ya uswahilini umenivutia kweli,

Kila niendapo natahamaki na jinsi watu wanavyo jibeba,

Maneno ya ukariimu,

Maadili na desturi za kistaarabu,

Heshma inayo sisimua roho,

Wabaki tu umesema MashaAllah,
La pili ni kuhusu mapenzi na uhusiano ya wapendanao,

Mapenzi yetu ipo Imara, ila yastahili kuimarika zaidi,

Nipe fursa na ruhusa niangalia ndani ya moyo wako,

Nipe fursa nione uchi wako,

Uchi wa mafikira na uwoga zote unazo, 

Ili niweze kukuonyesha vile nakupenda, 

Utakuta hakuna kitu cha kuficha ,

Pengine wataka kuficha kwa sababu ni wajibu wa kila mtu katika maisha yake,

Lakini nakusihi usiwe na ngao ukiwa na mimi,

Wajua linapokuja suala la kupendana basi mambo ya kuficha hakuna tena,

Kama una uhakika kuhusu uhusiano wako.
La Tatu la husu ndoa,

Unapopata tajriba hii, basi ushakamilisha nusu ya dini,

Nimeshapiga mbiu ya mgambo,

Kuwaeleza wazazi kuwa nishapata jiko,

Wiki ijayo, Majaaliwa, twaja kutoa posa,

Familia yako ni wandani wetu wa karibu,

Tuna matumaini hakuta kuwa na hamnazo mengi,

Mahari tukisha lipa, mimi na we tuanze safari mpya, 

Kuanzia hapo mimi na wewe mpaka milele,

Kwenye mabonde twende , baharini tuogelee hata hewani tutapaa .
Tukisubiri hayo nakusihii uchukuwe mda wako ufikirie,

Kama la wezekana tutafte ajira huku mombasa,

Kando na kupunguza gharama, ningefurahia kuishi nawe,

Naamini utafurahia huku, jiji la waisilamu tele,

Maadili ya wakaazi ni za kuvutia,

Nidhamu na desturi zao, watoto wetu pia wazipokee.

Uwa napata furaha sana kila ninapopata wasaa wa kukuandikia mpenzi,

Kikomo naishia hapa, mwisho wa barua moja ndio mwanzo wa barua nyingine nzuri na bora zaidi , kwahiyo usijali sana mrembo wangu,
Nakupenda sana mwandani wangu
Al Pacino

Leave a comment